Walimu Wa Uongo

Lakini pia walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyotokea walimu wa uongo kati yenu. Kwa siri, watain giza mafundisho ya upotovu hata kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watajiletea maangamizi ya haraka. Na wengi wata fuata tamaa zao potovu, na kwa ajili ya matendo yao njia ya kweli itadharauliwa. Nao katika tamaa yao watajaribu kuwanunua kwa kuwaambia hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu yao imekuwa tayari tangu zamani, wala mwangamizi wao hajalala usingizi.

Maana kama Mungu hakuwahurumia malaika walipotenda dhambi bali aliwatupa kuzimu, katika vifungo vya giza wakae huko mpaka siku ya hukumu; kama hakuuhurumia ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomcha Mungu, akamlinda Noe mjumbe wa haki, pamoja na watu saba wengine; kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza ikawa majivu, akaifanya kuwa mfano kwa wote ambao hawatamcha Mungu; na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki ambaye alihuzunishwa na maisha ya uchafu ya watu wahalifu - kwa sababu yale maasi aliyoona na kusikia huyo mtu wa Mungu alipoishi kati yao yalimhuzunisha usiku na mchana - basi ikiwa ni hivyo, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wa Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika hali ya adhabu mpaka siku ya hukumu. 10 Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa chafu za mwili na kudharau mamlaka. Watu hawa ni shupavu na katika kiburi chao, hawaogopi kuwatu kana viumbe vitukufu wa mbinguni;

11 ingawa hata malaika, ambao wana nguvu na uwezo zaidi, hawawashtaki au kuwatukana viumbe hao mbele za Bwana. 12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiy oyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawal iwa na hisia za mwili, ambao wamezaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa, na kama wanyama, wao pia wataangamizwa.

13 Watalipizwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Furaha yao ni kufanya karamu za ufisadi mchana, wazi wazi. Wao huleta aibu na fedheha wanaposhiriki katika karamu zenu kwa kuwa wakati wote huo, wanajifurahisha katika upotevu wao. 14 Macho yao yamejaa uzinzi, nao hutenda dhambi bila kikomo. Huwahadaa watu dhaifu. Mioyo yao imezoea kutamani. Hawa ni wana wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa kupata fedha kwa kufa nya maovu. 16 Balaamu alikaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena kwa sauti ya binadamu akamzuia huyo nabii asiendelee na kichaa chake.

17 Watu hawa ni kama chemchemi zilizokauka na ukungu upeper ushwao na tufani, na lile giza jeusi limewekwa tayari kwa ajili yao. 18 Wao hutamka maneno matupu ya majivuno na kutumia tamaa mbaya za mwili kuwanasa tena wale ambao ndio kwanza wameepukana na watu wanaoishi maisha ya uovu. 19 Huwaahidi hao waliowanasa kuwa watakuwa huru kabisa, lakini wao wenyewe ni watumwa wa upo tovu. Kwa maana mtu huwa mtumwa wa kitu kile kinachomshinda nguvu. 20 Kwa maana wale waliokwisha kuponyoka kutoka katika uchafu wa dunia hii kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo , kisha wakanaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. 21 Ingekuwa heri kwao kama hawa kuijua kamwe njia ya haki, kuliko kuifahamu kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyopewa. 22 Kama methali moja isemavyo, “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine, “Nguruwe huoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni.”

Walimu wa Uongo

Hapo zamani walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu wa Mungu. Ndivyo itakavyokuwa miongoni mwenu hata sasa. Watakuwepo walimu wa uongo katika kundi lenu, watakaoingiza mawazo yao wenyewe yatakayowaangamiza watu. Na watafundisha kwa werevu ambao mtashindwa kujua kuwa ni waongo. Watakataa hata kumtii Bwana aliwanunua. Na hivyo watajiangamiza haraka wao wenyewe. Watu wengi watawafuata katika mambo madaya ya kimaadili wanayotenda. Na kwa sababu yao, wengi wataikashifu njia ya kweli tunayoifuata. Manabii hawa wa uongo wanachotaka ni pesa zenu tu. Hivyo watawatumia ninyi kwa kuwaambia mambo yasiyo ya kweli. Lakini hukumu ya walimu hawa wa uongo imekwisha andaliwa kwa muda mrefu wala hawatakwepa. Mungu atawaangamiza, hajalala usingizi.

Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwaacha bila kuwaadhibu. Aliwatupia kuzimu. Aliwaweka malaika wale katika mapango yenye giza, wanakofungiwa mpaka wakati watakapohukumiwa na Mungu.

Na Mungu aliwaadhibu watu waovu walioishi zamani. Alileta gharika katika ulimwengu uliojaa watu waliokuwa kinyume na Mungu. Lakini alimwokoa Nuhu na watu wengine saba waliokuwa pamoja naye. Nuhu ndiye aliyewaambia watu kuhusu kuishi kwa haki.

Pia, Mungu aliiadhibu miji miovu ya Sodoma na Gomora. Aliichoma kwa moto mpaka kila kitu kikawa majivu. Alitumia miji hiyo kama mfano wa kile kitakachowapata watu walio kinyume na Mungu. Lakini alimwokoa Lutu, mtu mwema aliyeishi huko. Lutu aliugua sana moyoni kutokana na mwenendo wa kimaisha usiofaa na matendo ya uasi ya wale watu. Kila siku mtu huyu mwema aliishi miongoni mwa watu walioharibika, na moyo wake mwema uliumia kutokana na uhalifu na uvunjaji wa sheria aliyouona na kusikia.

Unaona namna ambavyo Mungu anajua kuwaokoa wale wanaomheshimu kutokana na matatizo yao. Na Bwana anajua jinsi ya kuwaweka watu waovu kifungoni hadi atakapowaadhibu siku ya hukumu. 10 Hukumu hiyo ni kwa wale ambao daima wanaofuata tamaa za udhaifu wao wa kibinadamu. Hiyo ni kwa ajili ya wale ambao wanadharau mamlaka ya Bwana.

Walimu hawa wa uongo hufanya chochote wanachotaka, na hujivuna sana. Wala hawaogopi kuwanenea mabaya viumbe wenye nguvu walioko angani. 11 Malaika wa Mungu ni hodari zaidi na wana nguvu kuliko viumbe hawa. Lakini hata hivyo malaika hao wa Mungu hawawatukani na kuwanenea mabaya viumbe hawa mbele za Bwana.

12 Lakini walimu hawa wa uongo wanasema uovu dhidi ya mambo wasiyoyaelewa. Wako kama wanyama ambao hufanya mambo bila ya kufikiri, ni kama wanyama wa porini waliozaliwa ili wakamatwe na kuuawa. Nao kama wanyama wataangamizwa. 13 Wamesababisha watu wengi kuteseka. Hivyo hata wao watateseka. Hayo ndiyo malipo yao kwa yale waliyofanya.

Wanadhani ni jambo la kufurahisha kutenda dhambi ambapo kila mtu anaweza kuwaona. Wanazifikiria sherehe zenye matendo yasiyofaa hata wakati wa mchana kweupe. Hivyo wao ni kama madoa ya uchafu na ni fedheha mnapokula pamoja nao. 14 Kila wakati wanapomwona mwanamke, wanamtamani na kumtaka. Wanatenda dhambi kwa njia hii daima. Na wanawasababisha wanyonge kutenda dhambi. Wamejifunza vyema wao wenyewe kuwa walafi. Wako chini ya laana.[a]

15 Walimu hawa wa uongo waliiacha njia sahihi na wakaiendea njia mbaya. Waliifuata njia ile ile aliyoifuata Balaamu. Alikuwa mwana wa Beori, aliyependa kulipwa kwa kufanya mabaya. 16 Alikemewa na punda kwa sababu alikuwa anatenda jamba baya. Punda alizungumza kwa sauti ya kibinadamu na akamzuia nabii yule kutenda kwa wazimu.

17 Walimu hawa wa uongo ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayosukumwa na dhoruba. Mahali penye giza nene pameandaliwa kwa ajili yao. 18 Wanajisifu kwa maneno yasiyo na maana. Wanawaongoza watu katika mitego ya dhambi. Wanawatafuta watu ambao wamechana na maisha ya kutenda dhambi na wanawarudisha tena katika kutenda dhambi. Wanafanya hivi kwa kutumia mambo ya aibu ambayo watu wanataka kuyatenda katika mapungufu yao ya kibinadamu. 19 Walimu hawa wa uongo wanawaahidi watu hao uhuru, lakini wao wenyewe hawako huru. Ni watumwa wa akili iliyoharibiwa na dhambi. Ndiyo, watu ni watumwa wa kitu chochote kinachowashinda.

20 Watu wanaweza kuwekwa huru ulimwenguni kutoka katika matendo ya aibu. Wanaweza kuyakwenda haya kwa kumwamini Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Lakini wakiyarudia maovu hayo na yakawatawala, hali yao inakuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni. 21 Ndiyo, ingekuwa bora kwao kutoijua kamwe njia sahihi. Ingekuwa bora kuliko kuijua njia sahihi kisha kugeuka kutoka katika mafundisho matakatifu waliyopewa. 22 Walichofanya ni kama “Mbwa anayekula matapishi yake.”(A) Na “Kama nguruwe aliyeoshwa, kisha anarudi kugaagaa matopeni.”

Footnotes

  1. 2:14 chini ya laana Kwa maana ya kawaida, “watoto wa laana”, ikimaanisha kuwa Mungu atawaadhibu.