17 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Majaribu yanayowafanya watu watende dhambi hayana budi kuwepo. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. Ingekuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito shingoni na kuzamishwa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. Kwa hiyo, jihadharini. Ndugu yako akikukosea mwonye; akiomba msamaha, msamehe. Hata kama akikuko sea mara saba kwa siku na kila mara aje kwako akisema, ‘Nisa mehe

Wanafunzi wakamwambia Bwana, “Tuzidishie imani.” Aka waambia, “Kama mngekuwa na imani kiasi cha punje ndogo sana ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu, ‘Ng’oka na mizizi yote ukaote baharini,’ nao ungewatii!”

Wajibu Wa Mtumishi

“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi aliyekwenda shambani kulima au kuchunga kondoo. Je, mtumishi huyo akirudi utamwambia, ‘Karibu keti ule chakula’? Hata kidogo. Badala yake utamwambia, ‘Nitayarishie chakula na ujiandae kunihudumia ninapokula na kunywa, na baada ya hapo unaweza kula chakula chako.’ Wala hutamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza wajibu wake. 10 Hali kadhalika nanyi, baada ya kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi ni watumishi tusiostahili, tumetimiza wajibu wetu tu.”’

Yesu Atakasa Wakoma Kumi

11 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu alipitia kati ya Samaria na Galilaya. 12 Alipokuwa akikaribia kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye. 13 Wakasimama mbali wakaita kwa nguvu, “Yesu! Bwana! tuonee huruma!” 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Na walipokuwa wakienda, wakapona ukoma wao. 15 Mmoja wao alipoona kwamba ame pona, akarudi kwa Yesu akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16 Kwa heshima kubwa akajitupa miguuni kwa Yesu akamshukuru. Yeye ali kuwa ni Msamaria .

17 Yesu akauliza, “Hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale tisa wengine? 18 Hakuna hata mmoja aliyekumbuka kurudi kumsifu Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 19 Akamwambia, “Inuka, uende; imani yako imekuponya.” Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja

20 Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa’ au ‘Ule kule’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona siku yangu moja, mimi Mwana wa Adamu lakini ham taiona. 23 Watu watawaambia, ‘Yule pale’ au, ‘Huyu hapa!’ Msiwa kimbilie. 24 Kwa maana kama umeme unavyomulika mbingu kutoka upande mmoja hadi mwingine, ndivyo itakavyokuwa siku ya kuja kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 25 Lakini kwanza itanipasa nite seke sana na kukataliwa na watu wa kizazi hiki. 26 Kama ilivy okuwa nyakati za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku ya kurudi kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 27 Wakati wa Nuhu watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo mafuriko yakaja yakawaangamiza wote. 28 Hata nyakati za Lutu ilikuwa hivyo hivyo. Watu walikuwa wakila, waki nywa, wakifanya biashara, wakilima na kujenga. 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, moto ulishuka kutoka mbinguni uka waangamiza wote. 30 Ndivyo itakavyokuwa siku ambapo mimi Mwana wa Adamu nitakapotokea kwa utukufu.

31 “Siku hiyo, mtu akiwa darini na vitu vyake vikiwa ndani, asiteremke kuvichukua. Hali kadhalika atakayekuwa shambani asi rudi nyumbani kuchukua cho chote. 32 Kumbukeni yaliyompata mke wa Lutu! 33 Mtu ye yote anayejaribu kusalimisha maisha yake atayapoteza; na ye yote atakayekuwa tayari kuyapoteza maisha yake atayaokoa. 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 35 Wana wake wawili watakuwa wanatwanga pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” [ 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.] 37 Wakamwuliza, “Haya yatatokea wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai wanapokutanika.” Mfano Wa Hakimu Dhalimu