Kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo. Mimi nimetumwa kwa wale ambao Mungu amewateua ili niwaon goze katika imani na katika maarifa ya kweli yanayopatana na kum cha Mungu; na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo. Naye kwa wakati aliopanga alidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo nilikabidhiwa kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.

Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu

Kazi Ya Tito Kule Krete

Nilikuacha huko Krete kusudi urekebishe mambo yote yal iokuwa hayakunyooka na uchague wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. Mzee wa kanisa asiwe na lawama yo yote; awe mume wa mke mmoja; awe ni mtu ambaye watoto wake ni waamini na wala sio jeuri au wasiotii. Kwa kuwa askofu amekabidhiwa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na lawama. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyokuwa ya halali. Bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye kujitawala, mnyofu, mtakatifu na mwe nye kudhibiti na si yake. Ni lazima alishike kwa uthabiti neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine na kudhihirisha makosa ya wale wanaolipinga.

Walimu Wa Uongo

10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.

16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.

Salamu kutoka kwa Paulo, mtumwa wa Mungu na mtume aliyetumwa na Yesu Kristo. Kazi yangu ni kuwasaidia wateule wa Mungu kumwamini Yeye zaidi na kuyaelewa kwa kina mafundisho ya Kristo. Mafundisho haya yatawaongoza kuishi katika njia inayomtukuza na kumpendeza Mungu. Na kisha wakatarajie kuishi pamoja na Mungu milele. Kabla ya mwanzo wa ulimwengu, Mungu aliahidi uzima wa milele kwa watu wake. Na wakati sahihi ulipotimia aliidhihirisha ile habari njema. Ujumbe huo ulikabidhiwa kwangu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu kumwambia kila mtu.

Nakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki:

Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu[a] Mwokozi wetu iwe nanyi.

Kazi ya Tito Krete

Nilikuacha kule Krete ili uweze kuyakamilisha yale yaliyokuwa yamebaki kufanyiwa kazi. Kisha nakuagiza uteue wazee na kuwaweka kuwa viongozi katika kila mji. Anayeweza kuteuliwa ni yule ambaye halaumiwi kwa matendo yoyote mabaya, na aliye mwaminifu kwa mkewe,[b] na anao watoto wanaoamini Mungu[c] na ambao sio wakaidi. Kwa sababu kila askofu,[d] anao wajibu wa kuitunza kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiyelaumiwa kwa kutenda mabaya yoyote. Asiwe mtu mkorofi. Asiwe mtu aliye mwepesi wa hasira. Asiwe mgomvi. Asiwe mtu mwenye kujipatia fedha toka kwa watu kwa njia ya udanganyifu. Mzee anapaswa kuwa mtu anayewakaribisha watu nyumbani mwake. Anapaswa kuyapenda yaliyo mema. Azingatie kuishi maisha yaliyo matakatifu. Na awe na uwezo wa kudhibiti nafsi yake. Anapaswa kuwa mwaminifu kwa ujumbe ule ule wa kweli tunaofundisha. Kwa namna hiyo ataweza kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya kweli na yenye manufaa.[e] Na ataweza kuwathibitishia wale wanaopinga mafundisho yake ya kuwa hawako sahihi.

10 Aina hii ya mafundisho ni muhimu kwa sababu wako watu wengi wasiopenda kumsikiliza mtu yeyote. Hao wanazungumzia mambo yao wenyewe yasiyo ya maana na kuwapotosha wengine waiache kweli. Ninaongelea hasa baadhi ya Wayahudi waaminio.[f] 11 Ni lazima wanyamazishwe kwani wanaivuruga jamii nzima kwa kufundisha mambo ambayo wasingepaswa kuyafundisha, lakini wanafanya hivyo ili kujipatia mapato yasiyo ya uaminifu! 12 Mmoja miongoni mwa watu wa kwao, Nabii kutoka Krete, alisema:

“Wakrete ni waongo daima.
    Si bora kuliko wanyama wa porini.
Daima wapo tayari kula,
    lakini hawapendi kufanya kazi.”

13 Usemi huu ni kweli, kwa hivyo wakaripie vikali ili wawe imara katika imani yao 14 na wasiendelee kuzisikilliza simulizi zinazopotosha za Kiyahudi na amri za wanadamu walioiacha kweli.

15 Kwa wale watu wenye mawazo yaliyo safi, kila kitu ni safi. Lakini hakuna kinachoweza kuwa safi kwa wasioamini ambao dhambi zao zimewafanya kuwa wachafu. Mawazo yao daima huwa yasiyo haki, na dhamiri zao pia zimekuwa chafu. 16 Hao hudai kuwa wanamjua Mungu, lakini matendo yao maovu yanaonesha kwa hakika kuwa hawamjui. Ni watu wenye kuchukiza mno na wasiotii, na hawafai kwa lo lote lililo jema.

Footnotes

  1. 1:4 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 1:6 mwaminifu kwa mkewe Kwa maana ya kawaida, “mtu mwenye mke mmoja”, yenye maana pia ameoa mara mmoja tu.
  3. 1:6 wanaoamini Mungu Neno hli laweza kuwa na maana ya “waaminifu” au “waaminio”. Hapa, maana zote zaweza kujumuishwa. Linganisha kifungu hiki na 1 Tim 3:4.
  4. 1:7 askofu Hapa ina maana, “mwangalizi” ama “mzee”. Tazama Mzee, Wazee katika Orodha ya Maneno.
  5. 1:9 ya kweli na yenye manufaa Kwa maana ya kawaida, “yaliyo sahihi”. Pia katika 2:1.
  6. 1:10 baadhi ya Wayahudi waaminio Kwa maana ya kawaida, “wale walio wa tohara”. Tazama Mdo 11:2; Gal 2:2.