Ujumbe Kwa Kanisa La Efeso

“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: ‘Haya ni maneno ya yule aliyeshika nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. Najua matendo yako, bidii yako na uvumilivu wako. Najua kuwa huwezi kuvumilia watu waovu na kwamba umewapima wale wanaojiita mitume na kumbe sio, na umetambua ya kuwa wao ni waongo. Najua umevumilia na kustahimili mateso kwa ajili ya jina langu, wala hujachoka .

Lakini nina neno hili juu yako: kwamba umeacha upendo wako wa kwanza. Kumbuka pale ulipokuwa kabla ya kuanguka. Tubu, uache dhambi zako, ukafanye matendo ya mwanzo. Kama hukuacha dhambi zako, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. Lakini una jambo moja zuri: unayachukia matendo ya Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.

Mwenye nia ya kusikia na ayasikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa . Atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ambao uko katika bustani ya Mungu.”’

Ujumbe Kwa Kanisa La Smirna

“Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye wa kwanza na wa mwisho; aliyekufa kisha akawa hai tena.

Naijua dhiki yako na umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri! Najua matukano wanayokutukana wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi; wao ni sinagogi la shetani. 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuhakikishia kuwa shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu. Nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

11 Mwenye nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa. Atakayeshinda hatadhuriwa na kifo cha pili.’ ”

Ujumbe Kwa Kanisa La Pergamo

12 “Kwa malaika wa Kanisa la Pergamo andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili.

13 Ninajua unakoishi, kule ambako shetani ameweka kiti chake cha enzi. Hata hivyo umelishika jina langu, wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambao ni maskani ya shetani.

14 Lakini nina mambo machache juu yako: baadhi yenu ni wafu asi wa mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki awashaw ishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na kufanya uasherati. 15 Na tena baadhi yenu wanafu ata mafundisho ya Wanikolai. 16 Basi tubuni mwache dhambi zenu: ama sivyo nitakuja hivi karibuni na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

17 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho ana waambia makanisa. Atakayeshinda nitampa sehemu ya ile mana iliy ofichwa, nami nitampa jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.’

Ujumbe Kwa Kanisa La Thiatira

18 “Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika hivi: ‘Haya ni maneno ya Mwana wa Mungu ambaye macho yake ni kama moto uwakao, na miguu yake inang’aa kama shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na subira yako; na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya mwanzo.

20 Hata hivyo ninalo jambo hili juu yako: unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kwa miungu. 21 Nimempa muda atubu, aache uasher ati, lakini hataki kutubu. 22 Kwa hiyo nitamtupa kitandani kwa ugonjwa, na atapata mateso makali pamoja na hao wanaozini naye wasipotubu matendo yake. 23 Tena nitawaua watoto wake. Ndipo makanisa yote yatajua kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na akili za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini ninawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamfuati mafundisho ya Yezebeli, wala ham kujifunza hayo wengine wanayoyaita ‘siri za ndani’ za shetani, sitawaongezea mzigo mwingine. 25 Bali mshike sana hicho mlicho nacho mpaka nitakapokuja.

26 Atakayeshinda na kuendelea kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa. 27 ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunja vipande vipande kama chombo cha udongo 28 Pia nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaambia makanisa.’ ”

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Efeso

“Andika hivi kwa malaika[a] wa kanisa lililoko Efeso:

Huu ni ujumbe kutoka kwake yeye anayeshikilia nyota saba katika mkono wake wa kulia na kutembea katikati ya vinara vya taa saba vya dhahabu.

Ninayajua matendo yako, unavyofanya kazi kwa bidii na usivyokata tamaa. Ninajua kwamba huwakubali watu waovu. Umewajaribu wote wanaojiita mitume lakini si mitume. Umegundua kuwa ni waongo. Huachi kujaribu. Umestahimili taabu kwa ajili ya jina langu na hujakata tamaa.

Lakini nina neno hili nawe umeuacha upendo uliokuwa nao hapo mwanzo. Hivyo kumbuka ulipokuwa kabla ya kuanguka. Ugeuze moyo wako na utende yale uliyoyatenda mwanzoni. Usipobadilika, nitakuja kwako na kutoa kinara chako cha taa mahali pake. Lakini unafanya vizuri kuyachukia matendo ya Wanikolai.[b] Mimi pia nayachukia mambo wanayotenda.

Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa. Wale watakaoshinda, nitawapa haki ya kula matunda kutoka kwenye mti wa uzima, ulio katika Bustani ya Mungu.

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Smirna

Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna:

“Huu ni ujumbe kutoka kwake aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa na akawa hai tena.

Ninayajua matatizo yako, na ninajua kwamba wewe ni maskini, lakini hakika wewe ni tajiri! Ninayajua matusi unayoteseka kutoka kwa watu wanaojiita Wateule wa Mungu.[c] Lakini si Wayahudi halisi. Watu hao ni wa kundi[d] la Shetani. 10 Usiogope mambo yatakayokupata hivi karibuni. Ninakwambia, Ibilisi atawafunga gerezani baadhi yenu ili kuipima imani yenu. Mtateseka kwa siku kumi, lakini iweni waaminifu, hata ikiwa mtatakiwa kufa. Mkiendelea kuwa waaminifu, nitawapa thawabu[e] ya uzima wa milele.

11 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa. Wale watakaoshinda hawatadhuriwa na mauti ya pili.

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Pergamo

12 Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo:

Huu ni ujumbe kutoka kwake aliye na upanga wenye makali kuwili unaotoka katika kinywa chake.

13 Ninapafahamu mahali unapoishi. Unaishi mahali kilipo kiti cha enzi cha Shetani, lakini wewe ni mwaminifu kwangu. Hukukataa kueleza kuhusu imani yako kwangu hata wakati wa Antipa. Antipa alikuwa shahidi wangu mwaminifu[f] aliyeuawa katika mji wako, mji ambao shetani anaishi.

14 Lakini nina vitu vichache kinyume nawe. Una watu huko wanaofuata mafundisho ya Balaamu. Balaamu alimfundisha Balaki namna ya kuwafanya watu wa Israeli kutenda dhambi. Walitenda dhambi kwa kula vyakula vilivyotolewa kwa ajili ya sanamu na kwa kufanya uzinzi. 15 Ndivyo ilivyo hata kwa kundi lako. Una watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai. 16 Hivyo igeuzeni mioyo yenu! Msipobadilika, nitakuja kwenu haraka na kupigana kinyume na watu hawa kwa kutumia upanga unaotoka katika kinywa changu.

17 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa!

Kila atakayeshinda nitampa mana iliyofichwa. Pia nitampa kila mshindi jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu yake. Na hakuna atakayejua jina hili isipokuwa yule atakayepata jiwe hili.

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Thiatira

18 Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira:

Huu ni ujumbe kutoka kwa Mwana wa Mungu, aliye na macho yanayong'aa kama moto na miguu kama shaba inayong'aa.

19 Ninayajua matendo yako. Ninajua kuhusu upendo wako, imani yako, huduma yako na uvumilivu wako. Ninajua kwamba unafanya zaidi sasa kuliko ulivyofanya kwanza. 20 Lakini ninalo hili kinyume nawe: Umemruhusu yule mwanamke Yezebeli afanye anachotaka. Anasema kwamba yeye ni nabii,[g] lakini anawapotosha watu wangu kwa mafundisho yake. Yezebeli huwaongoza watu wangu kutenda dhambi ya uzinzi na kula vyakula vilivyotolewa kwa sanamu. 21 Nimempa muda ili aubadili moyo wake na kuiacha dhambi yake, lakini hataki kubadilika.

22 Hivyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso. Na wale wote wanaozini naye watateseka sana. Nitafanya hivi sasa ikiwa hawataacha mambo anayofanya. 23 Pia, nitawaua wafuasi wake. Ndipo makanisa yote wataona kuwa mimi ndiye ninayefahamu kile ambacho watu wanadhani na kufikiri. Na nitamlipa kila mmoja wenu kutokana na kile alichotenda.

24 Lakini ninyi wengine mlioko Thiatira ambao hamjafuata mafundisho yake. Hamjajifunza mambo yanayoitwa ‘Siri za ndani za Shetani.’ Hivi ndivyo ninawaambia: Sitawatwika mzigo wowote. 25 Shikeni katika kweli mliyo nayo tu mpaka nitakapo kuja.

26 Nitawapa nguvu juu ya mataifa wale wote watakaoshinda na wakaendelea kutenda yale ninayotaka mpaka mwisho. 27 Watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma. Watayavunja vipande vipande kama vyombo vya udongo wa mfinyanzi.[h] 28 Watakuwa na nguvu ile ile niliyoipokea kutoka kwa Baba yangu, na nitawapa nyota ya asubuhi. 29 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa.

Footnotes

  1. 2:1 malaika Ama mwakilishi wa kanisa. Pia katika mstari wa 8,12 na 18 na pia katika barua zinazofuata Sura 3:1,7 na 14.
  2. 2:6 Wanikolai Kikundi cha kidini kilichofuata mafundisho ya uongo. Pia katika mstari wa 15.
  3. 2:9 Wateule wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “Wayahudi”. Pia katika 3:9.
  4. 2:9 kundi Kwa maana ya kawaida, “sinagogi”. Pia katika 3:9.
  5. 2:10 thawabu Kwa maana ya kawaida, “taji”, ni shada la majani au matawi ya miti lililowekwa juu ya vichwa vya washindi wa riadha ili kuwaheshimu. Ni alama inayoonyesha ushindi na zawadi.
  6. 2:13 shahidi wangu mwaminifu Mtu anayehubiri ujumbe wa Mungu kwa uaminifu, hata nyakati za hatari.
  7. 2:20 nabii Yezebeli alikuwa nabii mwongo. Alidai kuwa anazungumza kwa niaba ya Mungu, lakini hakuisema kweli ya Mungu.
  8. 2:26-27 Mistari hii inafanana na Zab 2:8-9 (tafsiri ya Kiyunani).