Wakaribisheni Wenye Imani Dhaifu

14 Kama mtu ana imani dhaifu mkaribisheni bila kubishana naye kuhusu maoni yake. Imani ya mtu mmoja inaweza kumruhusu kula kila kitu, ambapo mwingine ambaye imani yake ni dhaifu anakula mboga za majani tu. Mtu anayekula kila kitu asimhukumu yule asiyeweza kula kila kitu. Wala mtu ambaye hawezi kula kila kitu asimdharau yule anayekula kila kitu, kwa maana Mungu amemkubali. Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Ni bwana wake tu awezaye kuamua kama amesimama au ameanguka. Naye atasi mama kwa sababu Bwana anaweza kumfanya asimame.

Mtu mmoja anahesabu siku fulani kuwa ni bora kuliko nyin gine na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. Anayehesabu siku moja kuwa takatifu hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye anayekula nyama hufanya hivyo kwa kumtukuza Bwana, kwa maana humshukuru Mungu. Hali kadhalika akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa kum heshimu Bwana na humshukuru Mungu. Kwa maana hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe na wala hakuna hata mmoja wetu anayekufa kwa ajili yake mwenyewe. Kama tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana; na pia kama tukifa tunakufa kwa ajili ya Bwana. Kwa hiyo basi, kama tunaishi au kama tunakufa, sisi ni mali ya Bwana.

Maana kwa sababu hii, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi awe Bwana wa wote: waliokufa na walio hai.

10 Basi kwa nini unamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kumbuka kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11 Kwa kuwa imeandikwa:“Kama niishivyo, asema Bwana, Kila goti litapigwa mbele yangu, na kila ulimi uta mtukuza Mungu. 12 Kwa hiyo kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa

Usimkwaze Ndugu Yako

13 Basi, tuache kuhukumiana. Badala yake tuamue kuwa hatu tamkwaza ndugu kwa kitu cho chote. 14 Ninajua hakika kuwa nikiwa katika Bwana Yesu hakuna kitu cho chote ambacho kwa asili yake ni najisi. Lakini kwa mtu anayeamini kuwa kitu fulani ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15 Kama ndugu yako anahu zunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Usiruhusu kile ambacho unachokiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17 Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani na furaha ndani ya Roho Mtakatifu. 18 Kwa maana mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na anakubaliwa na wanadamu.

19 Kwa hiyo basi, tufanye kila juhudi tutimize yale yaletayo amani na kujengana. 20 Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Vyakula vyote vinafaa, lakini ni kosa kula kitu ambacho kinamfanya mwenzako kujikwaa. 21 Ni afadhali usile nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lo lote litakalomfanyandugu yako aanguke. 22 Unavyoamini kuhusu mambo haya, iwe ni siri yako na Mungu. Amebarikiwa mtu ambaye hajisikii kuhukumiwa afanyapo jambo analoamini kuwa ni sawa. 23 Lakini mtu mwenye mashaka kuhusu anachokula, amehukumiwa ikiwa atakula, kwa sababu kula kwake hakutokani na imani. Kwa maana jambo lo lote ambalo halito kani na imani, ni dhambi.

Msiwakosoe Wengine

14 Iweni tayari kuwakubali wenye mashaka kuhusu yale ambayo waamini wanaweza kufanya. Tena msibishane nao kuhusu mawazo yao tofauti. Baadhi ya watu wanaamini kuwa wanaweza kula aina yoyote ya chakula,[a] lakini wale walio na mashaka wanakula mboga za majani tu. Wale wanaojua kuwa wanaweza kula chakula cha aina yoyote hawapaswi kujisikia kuwa ni bora kuliko wale wanaokula mboga za majani tu. Na wale wanaokula mboga za majani tu hawapaswi kuamua kuwa wale wanaokula vyakula vyote wanakosea. Mungu amewakubali. Huwezi kuwahukumu watumishi wa mtu mwingine. Hilo linamhusu bwana wao mwenyewe ikiwa watafaulu au watashindwa. Na watakubaliwa, kwa sababu Bwana yuko tayari kuwafanya wafaulu.

Watu wengine wanaweza kuamini kuwa siku moja ni ya muhimu zaidi kuliko nyingine. Na wengine wanaweza kuwa na uhakika kuwa siku zote ziko sawa. Kila mtu anapaswa kujihakikisha juu ya imani yake katika akili zake wenyewe. Wale wanaofikiri kuwa siku moja ni ya muhimu kuliko siku zingine wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Na wale wanaokula vyakula vya aina zote wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Ndiyo, wanamshukuru Mungu kwa ajili ya chakula. Na wale wanaokataa kula vyakula fulani wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Nao pia wanamshukuru Mungu.

Hatuishi au kufa kwa ajili yetu sisi wenyewe tu. Kama tukiishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na kama tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Hivyo kuishi au kufa, sisi ni mali ya Bwana. Ndiyo sababu Kristo alikufa na kuishi tena ili awe Bwana juu ya wote waliokufa na wanaoishi.

10 Hivyo kwa nini unamhukumu kaka au dada yako katika familia ya Mungu? Au kwa nini unafikiri kuwa wewe ni bora kuliko wao? Sote tutasimama mbele za Mungu, naye atatuhukumu sisi sote. 11 Ndiyo, Maandiko yanasema,

“‘Hakika kama niishivyo’, asema Bwana,
    ‘kila mtu atapiga magoti mbele zangu,
    na kila mtu atasema kuwa mimi ni Mungu.’”(A)

12 Hivyo kila mmoja wetu ataeleza kuhusu matendo yake mbele za Mungu.

Msisababishe Wengine Wakatenda Dhambi

13 Hivyo tuache kuhukumiana sisi kwa sisi. Tuamue kutokufanya kitu ambacho kitasababisha matatizo kwa kaka au dada au kuathiri imani zao. 14 Najua kuwa hakuna chakula ambacho kwa namna yake chenyewe hakifai kuliwa. Bwana Yesu ndiye aliyenithibitisha juu ya jambo hilo. Lakini ikiwa mtu ataamini kuwa si sahihi kula chakula fulani, basi kwake yeye huyo hiyo haitakuwa sahihi akila chakula hicho.

15 Ikiwa utamuumiza kaka au dada yako kwa sababu ya chakula unachokula, hutakuwa unaifuata njia ya upendo. Kristo alikufa kwa ajili yao. Hivyo usiwaharibu kwa kula kitu wanachofikiri kuwa si sahihi kula. 16 Usiruhusu kile ambacho ni chema kwako kiwe kitu watakachosema ni kiovu. 17 Maisha katika ufalme wa Mungu siyo juu ya kile tunachokula na kunywa. Ufalme wa Mungu ni juu ya njia sahihi ya kuishi, amani na furaha. Vyote hii vinatoka kwa Roho Mtakatifu. 18 Yeyote anayemtumikia Kristo kwa kuishi namna hii anampendeza Mungu na ataheshimiwa na wengine.

19 Hivyo tujitahidi kwa kadri tuwezavyo kufanya kile kinacholeta amani. Tufanye kile kitakachomsaidia kila mtu kujengeka kiimani. 20 Msiruhusu kula vyakula kuiharibu kazi ya Mungu. Vyakula vyote ni sahihi kula, lakini ni makosa kwa yeyote kula kitu kinachomletea shida kaka au dada katika familia ya Mungu. 21 Ni heri kutokula nyama au kunywa divai au kufanya kitu chochote kinachoumiza imani ya kaka au dada yako.

22 Ilindeni imani yenu kuhusu mambo haya kama siri kati yenu na Mungu. Ni baraka kufanya kile unachofikiri ni sahihi bila kujihukumu mwenyewe. 23 Lakini ikiwa unakula kitu bila kuwa na uhakika kuwa ni sahihi, unakosea. Hii ni kwa sababu hukuamini kuwa ni sahihi. Na ukifanya chochote unachoamini kuwa si sahihi, hiyo ni dhambi.

Footnotes

  1. 14:2 aina yoyote ya chakula Sheria ya Kiyahudi ilisema kuwa kulikuwa na vyakula ambavyo Wayahudi wasingeweza kula. Walipofanyika wafuasi wa Kristo, baadhi yao hawakuelewa kuwa sasa wangeweza kula vyakula vyote.