Nafasi Ya Pekee Ya Waisraeli

Ninasema kweli katika Kristo na dhamiri yangu inanishuhudia kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwa sisemi uongo. Nina huzuni sana na uchungu usiokwisha moyoni mwangu. Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Kristo kama kufanya hivyo kungeweza kuwasaidia ndugu zangu tulio wa kabila moja. Nazungumza kuhusu Waisraeli ambao Mungu aliwateua kuwa wana wake, wakapewa utukufu wake, maagano yake, sheria yake, ibada ya kweli, na ahadi zake. Wao ni wa uzao wa mababu wa kwanza, na katika taifa lao Kristo alitoka kama mwanadamu; yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, atukuzwaye milele! Amina.

Lakini hii haina maana kwamba ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli imeshindwa. Kwa maana si wote ambao ni wa uzao wa Israeli ambao ni wa Israeli. Wala si wazaliwa wote wa kizazi cha Abra hamu ambao ni watoto wake. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ilikuwa: “Watoto wako watatoka katika uzao wa Isaki.” Kwa maneno men gine, si wale watoto waliozaliwa na Ibrahimu kimwili ambao ni wana wa Mungu; bali ni wale watoto wa ahadi ambao wanahesabiwa kuwa kizazi cha Abrahamu. Kwa maana ahadi yenyewe ilisema, “Nitarudi tena wakati kama huu na Sara atapata mtoto wa kiume.”

10 Na si hivyo tu bali pia wakati Rebeka alipozaa watoto na mume mmoja, Isaki, 11 hata kabla watoto wake mapacha hawajazal iwa wala kutenda jema au baya ili mpango wa Mungu wa kuchagua uendelee, si kwa kutegemea matendo mema bali kwa kufuatana na wito wake - 12 Rebeka aliambiwa, “Mkubwa atamhudumia mdogo.” 13 Kama Maandiko yasemavyo: “Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.”

Mungu Hana Upendeleo

14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.

19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?

22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa? 23 Na tunajuaje kama Mungu alifanya hivi ili kuwadhihirishia utajiri wa utukufu wake wale anaowahurumia, ambao aliwaandaa tangu mwanzo kupokea utu kufu? 24 Na sisi ndio hao walioitwa, si kutoka kwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko

25 Hivi ndivyo Mungu asemavyo katika kitabu cha Hosea, “Wale ambao hawakuwa watu wangu, nitawaita ‘watu wangu,’ na wale ambao hawakuwa wapendwa wangu, nitawaita ‘wapendwa wangu’.” 26 Na pale pale walipoambiwa,“Ninyi si ‘watu wangu,’ ndipo watakapoitwa, ‘Wana wa Mungu aliye hai’.” 27 Na Isaya anasema hivi kuhusu Israeli: “Ijapokuwa wana wa Israeli watakuwa wengi kama mchanga wa bahari, ni wachache tu miongoni mwao watakaooko lewa;

28 kwa maana Mungu ataitekeleza hukumu yakejuu ya ulimwengu mara moja na kuikamilisha.” 29 Na tena kama alivyotabiri Isaya,“Kama Bwana wa majeshi asingetuachia uzao, tungalikuwa kama Sodoma, na kufanywa kama Gomora.”

30 Kwa hiyo tusemeje basi? Watu wa mataifa ambao hawakuta futa kupata haki wamepewa haki kwa njia ya imani. 31 Lakini Waisraeli ambao wametafuta kupata haki kwa msingi wa sheria, hawakuipata kwa maana hawakutimiza sheria. 32 Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani bali kwa kutegemea matendo. Wali jikwaa kwenye lile ‘jiwe la kujikwaa.’ 33 Kama ilivyoandikwa kwe nye Maandiko,“Tazama naweka jiwe huko Sayuni ambalo linawafanya watu kujikwaa na mwamba utakaowaangusha, na wale watakaomtegemea hawataaibika kamwe.”

Mungu na Wayahudi

Nazungumza nayi sasa kama mmojawapo niliye wa Kristo. Hivyo mnaweza kuwa na uhakika kuwa sisemi uongo. Dhamiri yangu, inayotawaliwa na Roho Mtakatifu, inakubali kwamba ninayowaambia sasa ni kweli. Nimejawa na huzuni na maumivu ya moyoni yasiyokwisha kwa ajili ya watu wangu. Wao ni kaka na dada zangu katika mwili. Natamani ningeweza kuwasaidia. Ningekuwa tayari pia kuomba kupokea laana ya kutengwa na Kristo kama hiyo itaweza kuwasaidia. Ni Waisraeli, watoto waliochaguliwa na Mungu. Wameushuhudia utukufu wa Mungu na wanashiriki maagano aliyofanya Mungu na watu wake. Mungu aliwapa Sheria ya Musa, ibada ya Hekalu, na ahadi zake. Ni wazaliwa wa mababa zetu wakuu, na ni familia ya kidunia ya Masihi,[a] ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote. Yeye asifiwe milele![b] Amina.

Sina maana kuwa Mungu alishindwa kutimiza ahadi yake kwa Wayahudi. Lakini kwa hakika ni baadhi tu ya Waisraeli ndiyo watu wa Mungu[c]. Na hivyo ni baadhi tu ya watoto wa Ibrahimu ndiyo wazaliwa wake halisi. Hivi ndivyo Mungu alimwambia Ibrahimu: “Wazaliwa wako halisi watakuwa wale waliotoka kwa Isaka.”(A) Hii ina maana kuwa si watoto wote wa Ibrahimu walio watoto halisi wa Mungu. Wazaliwa halisi wa Ibrahamu ni wale wanaofanyika watoto wa Mungu kwa sababu ya agano ambalo Mungu alililiweka na Ibrahamu. Hivi ndivyo Mungu alivyosema katika agano hilo: “Wakati kama huu mwaka ujao nitakujia tena, na Sara mke wako atazaa mwana.”(B)

10 Na si hivyo tu. Kitu kama hicho kilimtokea Rebeka ambaye baada ya kupata mimba ya wana wawili mapacha waliotokana na baba mmoja, baba yetu Isaka. 11-12 Ndiyo, kabla ya kuzaliwa wana hao mapacha, Mungu alimwambia Rebeka, “Mwana mkubwa atamtumikia mdogo.”(C) Hii ilikuwa kabla wavulana hawa hawajatenda jambo lolote jema au baya. Mungu alisema hivi kabla hawajazaliwa ili kwamba mvulana ambaye Mungu alimtaka atachaguliwa kutokana na mpango wa Mungu mwenyewe. Mvulana huyu alichaguliwa kwa sababu ndiye ambaye Mungu alitaka kumwita, si kwa sababu ya jambo lolote walilofanya wavulana hao. 13 Kama Maandiko yanavyosema, “Nilimpenda Yakobo lakini nilimchukia Esau.”(D)

14 Namsikia mtu akiuliza, “Hivyo hii ina maana gani? Je, Mungu si mwenye haki?” Hapana! 15 Mungu alimwambia Musa, “Nitampa rehema yeyote ninayetaka kumpa rehema. Nitamhurumia yeyote ninayemchagua.”(E) 16 Hivyo Mungu atamchagua yeyote anayeamua kumpa rehema pasipo kujali watu wanataka nini ama kwa jinsi gani wanapiga mbio. 17 Katika Maandiko Mungu anamwambia Farao: “Nilikuweka uwe mfalme kwa kusudi hili hasa: kuonesha nguvu zangu kupitia kwako. Nilitaka jina langu litangazwe ulimwenguni kote”(F) 18 Hivyo Mungu huwarehemu wale anaotaka kuwarehemu na huwafanya jeuri wale anaotaka wawe jeuri.

19 Hivyo utaniuliza, “Ikiwa unayosema ni kweli, kwa nini Mungu amlaumu mtu yeyote kwa kufanya makosa? Hayupo anayeweza kukataa kufanya yale anayotaka Mungu, Je, yupo?” 20 Hilo si la kuuliza. Wewe ni mwanadamu tu na huna haki ya kumhoji Mungu. Chungu hakiwezi kumhoji aliyekifinyanga. Hakiwezi kusema, “Kwa nini ulinifinyanga hivi?” 21 Yeye aliyefinyanga chungu anaweza kufinyanga kitu chochote anachotaka. Anautumia udongo ule ule wa mfinyanzi kufinyanga vitu mbalimbali. Anaweza kufinyanga kitu kimoja kwa makusudi maalumu na kingine kwa matumizi ya kila siku.

22 Ni kwa jinsi hiyo hiyo Mungu amefanya. Alitaka kuionesha hasira yake na kuwafanya watu waone nguvu zake. Lakini kwa uvumilivu wake aliwastahimili wale waliomuudhi, watu waliokuwa tayari kuangamizwa. 23 Alingoja kwa uvumilivu ili aweze kuutangaza utajiri wa utukufu wake kwa watu aliowachagua wapokee rehema zake. Mungu alikwisha waandaa kuushiriki utukufu wake. 24 Sisi ndiyo watu hao, ambao Mungu alituchagua si tu kutoka kwa Wayahudi lakini pia kutoka kwa wale wasio Wayahudi. 25 Kama Mungu anavyosema katika kitabu cha Hosea,

“Watu wasiokuwa wangu,
    nitasema ni watu wangu.
Na watu ambao sikuwapenda,
    nitasema ni watu ninaowapenda.(G)
26 Na pale Mungu aliposema zamani:
‘Ninyi si watu wangu’;
    hapo wataitwa watoto wa Mungu aliye hai.”(H)

27 Na Isaya huililia Israeli:

“Wako watu wengi sana wa Israeli,
    kuliko mchanga ulio pwani ya baharini.
    Lakini wachache wao watakaookolewa.
28 Ndiyo, Bwana atakamilisha kwa haraka
    aliyosema atayafanya duniani.”(I)

29 Ni kama vile alivyosema Isaya:

“Ikiwa Bwana Mwenye Uweza wote
    asingewaruhusu watu wachache wakaishi,
tungekuwa tumeangamizwa kabisa,
    kama vile miji miovu ya Sodoma, na Gomora.”(J)

30 Hivyo haya yote yanamaanisha nini? Je, tunasema kwamba watu wasio Wayahudi walifanikiwa kukipata kibali cha Mungu, hata kama hawakuwa wakijaribu kukipata kibali hicho? Ndiyo. Walipata kibali hicho kwa sababu ya imani kwa Mungu. 31 Na vipi kuhusu watu wa Israeli? Wao walitaka kujipatia kibali cha Mungu kwa kuifuata sheria. Je, tunasema kuwa hawakufanikiwa? 32 Ndiyo, na sababu yake ni hii: Walijitahidi kukipata kwa kufanya kwa usahihi mambo yote yaliyoamriwa katika sheria badala ya kumtumaini Mungu. Walijikwaa kwenye jiwe linalowafanya watu waanguke. 33 Maandiko yanazungumza kuhusu jiwe hilo:

“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni litakalowafanya watu wajikwae.
    Ni mwamba utakaowaangusha watu.
Lakini yeyote atakayemtumaini yeye
    hataaibika kamwe.”(K)

Footnotes

  1. 9:5 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Kristo”, tafsiri ya Kiyunani kwa neno “Masihi”. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 9:5 Masihi, ambaye … milele Au “Masihi. Mungu, anayevitawala vitu vyote, asifiwe milele!”
  3. 9:6 watu wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “Israeli”, watu aliowachagua Mungu ili kuleta baraka ulimwenguni.