Mfano Wa Abrahamu

Tusemeje basi kuhusu baba yetu Abrahamu? Yeye alijifunza nini? Ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, basi anacho kitu cha kujivunia, lakini si mbele za Mungu. Maandiko yanase maje? “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa ajili ya imani yake aka hesabiwa haki.”

Mtu akifanya kazi, mshahara wake hauhesabiwi kuwa ni zawadi bali ni haki yake. Lakini kwa mtu ambaye hakufanya kazi ila amemtegemea Mungu anayewahesabia haki waovu, imani yake inahesabiwa kuwa haki. Daudi pia ana maana hiyo hiyo anapoongea juu ya baraka apatazo mtu ambaye Mungu amemhesabia haki pasipo kutenda lo lote: “Wamebarikiwa wale ambao makosa yao yamesame hewa, ambao dhambi zao zimefunikwa. Amebarikiwa mtu ambaye Bwana hamhesabii dhambi zake.”

Haki Kabla Ya Tohara

Je, baraka hii anayosema Daudi ni ya wale waliotahiriwa tu au pia ni ya wale wasiotahiriwa? Tunasema kwamba imani ya Abra hamu ilihesabiwa kama haki. 10 Je, hii ilitokea wakati gani? Je, ilikuwa ni kabla au baada ya kutahiriwa kwake? Haikuwa baada, ila kabla hajatahiriwa. 11 Na alipewa tohara kama alama na mhuri wa haki aliyoipokea kwa imani hata kabla ya kutahiriwa. Shabaha ya Mungu ilikuwa kwamba Abrahamu awe baba ya wote wenye imani ambao bado hawajatahiriwa ili wao pia wahesabiwe haki. 12 Pia yeye ni baba wa wale waliokwisha kutahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani aliyokuwanayo baba yetu

Haki Haipatikani Kwa Sheria

13 Ahadi ambayo Mungu alimpa Abrahamu na kizazi chake, kwamba ataurithi ulimwengu, haikutolewa kwa kuwa Abrahamu alitii sheria lakini ni kwa sababu alikuwa na imani, na Mungu akaihesabu imani yake kuwa ni haki. 14 Ikiwa wafuatao sheria tu ndio wata kaopewa urithi ulioahidiwa na Mungu, basi imani si kitu na ahadi hiyo haina thamani. 15 Kwa maana sheria huleta ghadhabu ya Mungu na ambapo hakuna sheria basi hakuna makosa.

16 Ndio maana ahadi hiyo ilitolewa kwa msingi wa imani, ili ipatikane bure kwa neema na ithibitishwe kwa vizazi vyote vya Abrahamu, si wale tu walio na sheria, bali pia na wale wenye imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sote. 17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu aliyemwamini. Mungu ambaye ana wapa wafu uhai na ambaye huamuru vitu ambavyo havipo viwepo.

Mfano Wa Imani Ya Abrahamu

18 Ijapokuwa ilionekana kama matumaini ya Ibrahimu yalikuwa ya bure, yeye alimtumaini na kumwamini Mungu na kwa kufanya hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyokuwa ameahidiwa kwamba, “Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.” 19 Ijapokuwa mwili wake hau kuwa tena na uwezo wa kuzaa, alikuwa na umri upatao miaka mia moja na Sara alishapita umri wa kuzaa, imani yake haikufifia. 20 Abrahamu hakuacha kuamini wala hakuwa na mashaka juu ya ahadi ya Mungu. Imani yake ilimtia nguvu, akamtukuza Mungu, 21 akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza ali loahidi. 22 Ndio sababu imani yake, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.” 23 Maneno haya, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki,” hay akuandikwa kwa ajili yake peke yake 24 bali kwetu pia. Tutahe sabiwa haki sisi tunaomwamini Mungu aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka kwa wafu. 25 Yesu aliuawa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuliwa ili tuhesabiwe haki.