Uhai Katika Kristo

Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka? Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi, tuendelee tena kuishi humo? Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? Kwa hiyo tulikufa na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate kuishi maisha mapya.

Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake. Tunafahamu kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena. 10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi anamwishia Mungu.

11 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kujihesabu kuwa wafu kwa mambo ya dhambi bali hai kwa Mungu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.

12 Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ambayo ni ya muda, iwafanye mzifuate tamaa za mwili. 13 Msiku bali kutoa sehemu yo yote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu zitumike kama vyombo vya haki. 14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa na neema. Watumwa Wa Haki

15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa hatutawa liwi na sheria bali tuko chini ya neema? La , sivyo! 16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa wa utii ambao huleta haki. 17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao mlikuwa watumwa wa dhambi mmetii kwa moyo wote mafundi sho mliyopewa. 18 Mmewekwa huru, mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa haki. 19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.

20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21 Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni kifo. 22 Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru kutokana na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakaso, na hatimaye, uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.