Kifo Cha Lazaro

11 Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika kijiji cha Bethania pamoja na dada zake wawili, Mariamu na Martha. Huyu Mariamu ndiye aliyempaka Bwana Yesu manukato miguuni na kumpangusa kwa nywele zake. Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” Lakini Yesu alipopata habari hizi alisema, “Ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea ili kudhihirisha utu kufu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi Mwana wa Mungu, nitatukuzwa. ”

Kwa hiyo ijapokuwa Yesu aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro, alipopata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukaa huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea.” Wanafunzi wake wakam wambia, “Mwalimu, utakwendaje tena Yudea ambako siku chache tu zilizopita Wayahudi walitaka kukupiga mawe?” Yesu akawajibu, “Si kuna masaa kumi na mawili ya mchana katika siku moja? Mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa maana kuna mwanga wa ulim wengu. 10 Lakini mtu akitembea usiku hujikwaa kwa sababu hana mwanga nafsini mwake.”

11 Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”

Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.” 13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi. 14 Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa. 15 Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla Lazaro kufa. Hii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni.” 16 Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe pamoja naye.”

Yesu Ni Ufufuo Na Uzima

17 Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita. 18 Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu, 19 Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. 20 Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani. 21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa. 22 Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.” 23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.” 24 Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; 26 na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?” 27 Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.”

Yesu Analia

28 Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita.” 29 Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu. 30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye. 31 Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata. 32 Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.” 33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34 akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” 35 Yesu akalia. 36 Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!” 37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”

Yesu Amfufua Lazaro

38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. 39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. 42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.” 43 Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”

Mpango Wa Kumwua Yesu

45 Wayahudi wengi waliokuja kumfariji Mariamu, walipoona yaliyotokea wakamwamini Yesu. 46 Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya. 47 Kwa hiyo maku hani wakuu na Mafarisayo wakafanya baraza wakaulizana, “Tufa nyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48 Kama tukimruhusu aendelee hivi, kila mtu atamwamini; na Warumi watakuja kuharibu Hekalu letu na taifa letu.” 49 Lakini mmoja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu kwa mwaka ule akawaambia wen zake, “Ninyi hamjui kitu! 50 Hamwoni kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, badala ya taifa lote kuangamia?” 51 Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka ule, alikuwa anatabiri kuwa Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi; 52 na pia kwa ajili ya watoto wa Mungu wal iotawanyika ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53 Tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu. 54 Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani, bali alitoka Bethania akaenda mikoani karibu na jangwa, kwenye kijiji kimoja kiitwacho Efraimu. Alikaa huko na wanafunzi wake.

55 Wakati Pasaka ya Wayahudi ilipokaribia, watu wengi wali toka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajita kase kabla ya sikukuu. 56 Watu walikuwa wakimtafuta Yesu, wakawa wanaulizana wakati wamesimama Hekaluni, “Mnaonaje? Mnadhani ata kuja kwenye sikukuu?” 57 Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa kama yupo mtu anayefahamu alipo awafahamisha, ili wapate kumkamata.