Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu

Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyet enda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”

Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”

Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona!

Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona akiomba omba wakauliza, “Huyu si yule kipofu aliyekuwa akiketi hapa akiomba msaada?” Baadhi wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “Siye, bali wamefanana.” Lakini yeye akawahakikishia kuwa yeye ndiye yule kipofu ambaye sasa anaona.

10 Wakamwuliza, “Macho yako yalifumbuliwaje?” 11 Akawaam bia, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope akanipaka machoni akaniambia niende nikaoshe uso katika kijito cha Siloamu. Nikaenda na mara baada ya kuosha uso nikaweza kuona!” 12 Wakam wuliza, “Huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.”

Mafarisayo Wachunguza Kuponywa Kwa Kipofu

13 Wakampeleka yule mtu aliyeponywa upofu kwa Mafarisayo. 14 Siku hiyo Yesu aliyomponya ilikuwa siku ya sabato. 15 Mafar isayo nao wakamwambia awaeleze jinsi alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho, nikanawa uso na sasa naona.” 16 Baadhi ya Mafarisayo wakamwambia, “Huyu mtu ali yekuponya hawezi kuwa ametoka kwa Mungu kwa sababu hatimizi she ria ya kutokufanya kazi siku ya sabato.” Lakini wengine wakab isha, wakiuliza, “Anawezaje mtu mwenye dhambi kufanya maajabu ya jinsi hii?” Pakawepo na kutokuelewana kati yao . 17 Kwa hiyo wakamgeukia tena yule aliyeponywa wakamwuliza, “Wewe unamwonaje huyu mtu ambaye amekufanya ukaweza kuona?” Yeye akawajibu, “Mimi nadhani yeye ni nabii.”

18 Wale viongozi wa Wayahudi hawakuamini ya kuwa yule mtu aliwahi kuwa kipofu, mpaka walipoamuru wazazi wake waletwe; 19 wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu ambaye alizaliwa kipofu? Ikiwa ndiye, imekuwaje sasa anaweza kuona?” 20 Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu ambaye ali zaliwa kipofu. 21 Lakini hatujui jinsi alivyoponywa akaweza kuona, wala hatujui ni nani aliyemwezesha kuona. Mwulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” 22 Walisema hivi kwa tahadhari kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wamekubal iana kuwa mtu ye yote atakayetamka kuwa Yesu ndiye Kristo atafu kuzwa kutoka katika ushirika wa sinagogi. 23 Ndio maana wakasema “Mwulizeni, yeye ni mtu mzima.”

24 Kwa hiyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu wakamwambia, “Tuambie kweli mbele ya Mungu. Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.” 25 Akawajibu, “Kama yeye ni mwenye dhambi au sio, mimi sijui. Lakini nina hakika na jambo moja: nil ikuwa kipofu na sasa naona.”

26 Wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” 27 Akawajibu, “Nimekwisha waambia aliyonifanyia lakini hamtaki kusikia. Mbona mnataka niwaeleze tena? Au na ninyi mna taka kuwa wafuasi wake?” 28 Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ni mfuasi wake. Sisi ni wafuasi wa Musa. 29 Tunajua kwamba Mungu alisema na Musa. Lakini huyu mtu hatujui anakotoka.” 30 Akawa jibu, “Hii kweli ni ajabu! Hamjui anakotoka naye ameniponya upofu wangu! 31 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomwabudu na kumtii. 32 Haijawahi kutokea tangu ulimwengu kuumbwa kwamba mtu amemponya kipofu wa kuzaliwa. 33 Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufa nya lo lote.” 34 Wao wakamjibu, Wewe ulizaliwa katika dhambi! Utawezaje kutufundisha?” Wakamfukuzia nje.

Vipofu Wa Kiroho

35 Yesu alipopata habari kuwa yule mtu aliyemfumbua macho amefukuzwa kutoka katika sinagogi, alimtafuta akamwuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?” 36 Yule mtu akamjibu, “Tafadhali nifahamishe yeye ni nani ili nipate kumwamini.” 37 Yesu akam jibu “Umekwisha mwona naye ni mimi ninayezungumza nawe.” 38 Yule mtu akamjibu huku akipiga magoti, “Bwana, naamini.”

39 Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu; ili wale walio vipofu wapate kuona; na wale wanaodhani wanaona, waonekane kuwa vipofu.”

40 Baadhi ya Mafarisayo waliomsikia akisema hivi wakauliza, “Je, unataka kusema kuwa sisi pia ni vipofu?” 41 Yesu akawa jibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, hamngekuwa na hatia. Lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi bado mna hatia.”