Add parallel Print Page Options

Mwanamke Ampa Yesu Heshima

(Mt 26:6-13; Mk 14:3-9)

12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alienda Bethania. Huko ndiko alikoishi Lazaro, yule mtu aliyefufuliwa na Yesu kutoka wafu. Hapo walimwandalia Yesu karamu ya chakula. Naye Martha alihudumu na Lazaro alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakila chakula pamoja na Yesu. Mariamu akaleta manukato ya thamani sana yaliyotengenezwa kwa nardo asilia kwenye chombo chenye ujazo wa nusu lita[a] hivi. Akayamwaga manukato hayo miguuni mwa Yesu. Kisha akaanza kuifuta miguu ya Yesu kwa nywele zake. Harufu nzuri ya manukato hayo ikajaa nyumba nzima.

Yuda Iskariote, mmoja wa wafuasi wa Yesu, naye alikuwepo hapo. Yuda ambaye baadaye angemkabidhi Yesu kwa maadui zake akasema, “Manukato hayo yana thamani ya mshahara wa mwaka[b] wa mtu. Bora yangeuzwa, na fedha hizo wangepewa maskini.” Lakini Yuda hakusema hivyo kwa vile alikuwa anawajali sana maskini. Alisema hivyo kwa sababu alikuwa mwizi. Naye ndiye aliyetunza mfuko wa fedha za wafuasi wa Yesu. Naye mara kadhaa aliiba fedha kutoka katika mfuko huo.

Yesu akajibu, “Msimzuie. Ilikuwa sahihi kwake kutunza manukato haya kwa ajili ya siku ya leo; siku ambayo maziko yangu yanaandaliwa. Nyakati zote mtaendelea kuwa pamoja na hao maskini.[c] Lakini si kila siku mtakuwa pamoja nami.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 12:3 nusu lita Kwa maana ya kawaida, “litra” ni ratili ya Kirumi, sawa na gramu 327.
  2. 12:5 mshahara wa mwaka Wa mwaka wa mtu kwa hali halisi “dinari 300” (sarafu za fedha). Sarafu moja, dinari ya Kirumi, ilikuwa ni wastani wa mshahara wa mtu wa siku moja.
  3. 12:8 maskini Nyakati zote wataendelea kuwepo maskini pamoja nanyi. Tazama Kum 15:11.