Add parallel Print Page Options

Yesu Afariki

(Mt 27:45-56; Lk 23:44-49; Yh 19:28-30)

33 Ilipofika saa sita mchana giza ilifunika nchi yote. Giza liliendelea hadi saa tisa. 34 Mnamo saa tisa Yesu alipiga kelele kwa sauti na kusema, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”(A)

35 Na baadhi ya wale waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hivi, walisema, “sikilizeni anamwita Eliya.”[a]

36 Mtu mmoja alikimbia na kujaza sifongo kwenye siki, akaliweka kwenye ufito, na akampa Yesu anywe akisema, “Subiri! Tuone ikiwa Eliya atashuka na kumshusha chini.”

37 Yesu akalia kwa sauti kubwa na kisha akafa.

38 Hapo pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili kutoka juu hadi chini. 39 Yule afisa wa jeshi aliyekuwa amesimama pale mbele na kuona jinsi Yesu alivyokufa. Afisa huyu alisema, “mtu huyu hakika alikuwa mwana wa Mungu!”

40 Baadhi ya wanawake walikuwa wakiangalia mambo haya toka mbali. Miongoni mwao alikuwapo Maria Magdalena, Salome, na Maria mama yake Yakobo na Yose. 41 Wanawake hawa ni wale waliomfuata Yesu huko Galilaya na kumhudumia. Wanawake wengi wengine waliofuatana naye kuja Yerusalemu walikuwapo pale pia.

Read full chapter

Footnotes

  1. 15:35 anamwita Eliya Neno hili “Mungu wangu” (ni Eli kwa Kiebrania ama Eloi kwa Kiaramu) ilisikika kwa watu kama jina la Eliya. Nabii maarufu aliyeishi mikaka kama 850 KK.